Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaandaa uvumbuzi mpya wa kitaalamu.

Maoni katika picha
Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaa/26 Hashdi Shaábi) kimeandaa kongamano chini ya usimamizi wa kiongozi wake mkuu Shekh Maitham Zaidi, na kuhudhuriwa na makamanda na wakuu wa vikosi vyake.

Wakuu wa vikosi wametoa wito wa kuimarisha mawasiliano na vikosi vingine vya Hashdi Shaábi, na kumsaidia kila anayetaka kuimarisha jambo hilo, pamoja na kuendelea kutoa mafunzo na kubuni mitambo ya kitaalamu, aidha kongamano hili linaangalia mahitaji ya wapiganaji sambamba na kuangalia namna ya kusaidia familia za mashahidi na majeruhi.

Kikosi kimesema kua kipo mbioni kufanya uvumbuzi wa kitaalamu kupitia kituo cha utafiti na uendelezaji kilicho chini yake, ndani ya miezi miwili ijayo, kifaa hicho kitakabidhiwa kwa moja ya mashirika ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kitakua na nafasi kubwa ya kutibu matatizo wanayo pata wakulima katika mkoa wa Karbala, tunategemea kukisambaza na kukigawa kwenye mikoa mingine katika misimu ijayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: