Marjaa Dini mkuu bado anaendelea kusisitiza maandamano ya amani, na kujiepusha na vitendo vya ukatili, na kwamba jambo hilo ni muhimu sana, akasema kua hilo ni jukumu la wote, aidha akazungumza jambo lingine muhimu ni vyombo vya ulinzi na usalama kuwalinda watu wanaofanya maandamano ya amani, hali kadhalika waandamanaji wasiwashambulie askari au mali za umma.
Aliyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa mwezi (9 Rabiu Thani 1441h) sawa na (6 Novemba 2019m) katika haram ya Imamu Hussein (a.s) iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Kufanya maandamano ya amani na kujiepusha na vitendo vya ukatili na uharibifu ni muhimu sana, nalo ni jukumu la kila mtu, kama ilivyo wajibu kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwalinda watu wanaofanya maandamano ya amani na kuwapa nafasi ya kuwasilisha madai yao kwa uhuru, hali kadhalika waandamanaji hawatakiwi kuwapa nafasi watu waovu kuingia kwenye maandamano yao na kuwashambulia askari na mali za umma, kwani jambo hilo lina madhara makubwa kwa wananchi).