(Nibrasu Anwaru fi Abbasi Akbaru) anaona nuru.

Maoni katika picha
Toleo jipya katika kituo cha masomo ya kitafiti kuhusu Abulfadhil Abbasi (a.s), kitabu kiitwacha (Nibrasu Anwaru fi Abbasi Akbaru) kilicho beba kurasa zinazo elezea sira ya mwezi wa bani Hashim (a.s) katika sekta tofauti, kimeandikwa kisasa na kunukuu maoni ya watafiti wa zamani na hoja zao pamoja na kutoa maoni ya mtazamo wa kielimu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kituo hicho kitabu kinakurasa karibu elfu moja na kina juzuu tatu na milango saba ambayo muandishi ameiita taa, kama ifuatavyo:

Kwanza habari zake na wasifu wake kitabia na kimaumbile, pili familia yake, tatu mama yake Ummul Banina (a.s), nne ndugu zake kwa baba na mama, tano katika familia yake, sita kuhusu habari zake (a.s) katika vita ya Twafu, saba mwisho na hatima ya maneno.

Kumbuka kua kitabu hiki ni moja ya vitabu vilivyo tolewa na kituo, kinamada mbalimbali chini ya jina la Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuingiza katika maktaba za kiislamu nakala zinazo muelezea mtukufu huyu na jinsi alivyo jitolea, kwa mahitaji ya kitabu hiki na vingine unaweza kutembelea maonyesho yetu ya vitabu katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: