Yalisemwa na Marjaa: Tunaunga mkono maandamano ya amani na tunapinga kushambuliwa waandamanaji au vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na mali za umma na binafsi.

Maoni katika picha
Toka yalipoanza maandamano hapa Iraq ya kudai islahi na kurudisha haki zilizo vunjwa, yaliyo sambaa kwenye mikoa tofauti ya Iraq, Marjaa Dini mkuu alitangaza msimamo wake kuhusu maandamano hayo aliyoyaita vita ya islahi, akayaunga mkono na akasisitiza yafanywe kwa amani na kujiepusha na vitendo vya ukatili na uharibifu.

Katika kutilia mkazo msimamo wake huo khutuba ya Ijumaa ya (17 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (15/11/2019m, akazungumza maneno hayo kupitia muwakilishi wake Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatali ni tamko kuhusu swala hilo:

(Tunaunga mkono maandamano ya amani na tunahimiza kujiepusha na kuwashambulia watu wanaofanya maandamano ya amani kwa kuwaua, kuwapiga au kuwateka na mengineyo, aidha tunalaani kushambuliwa askari na mali za umma na binafsi, kila atakaye fanya hivyo inatakiwa achukuliwe hatua kwa mujibu wa sharia, wala haifai kufumbiwa macho mambo hayo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: