Harakati za kituo cha Swidiqah Twahirah katika siku za kukumbuka kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Kituo cha Swidiqah Twahira (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa harakati zake za kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s) siku za huzuni ya Fatwimiyya zilizo anza tangu siku ya kwanza na zikaendelea kwa muda wa siku tatu.

Kiongozi wa kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) bibi Zainabu Ardawi ameongea na mtandao wa Alkafeel kua: “Katika muendelezo wa harakati zinazo ratibiwa na kituo cha Swidiqah Twahirah chini ya Ataba tukufu, miongoni mwa harakati hizo ni kufanya majlisi za kuomboleza kifo cha bibi Swidiqatu Kubra Fatuma Zaharaa (a.s)”. akaongeza kua: “Majlis zilikua na mihadhara kuhusu hutuba za bibi Fatuma (a.s) zinazo onyesha msimamo wake mtukufu na nafasi ya mwanamke katika kutetea haki kwa kufuata masharti na taratibu zake, zilizo weka mzani wa mwenendo unaofuatwa na Ahlulbait (a.s) na Fatuma Zaharaa (a.s), ni njia muhimu ya kutetea haki na kufanya islahi, katika zama zetu wanawake wanatakiwa kufuata nyayo za bibi Zaharaa (a.s) kutoka kwake ilikua hatua ya kwanza ya kutatua matatizo ya umma katika zama zake (a.s) hadi leo.

Akabainisha kua: “Harakati zetu hazikuishia hapo tulikua na shughuli zingine za kijamii na kitamaduni kuhusu mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kulikua na majlis za kuomboleza za watoto, kituo kiliandaa majlis zinazo endana na mahala pamoja na uwezo wa watoto wa kumtambua bibi Zaharaa (a.s) na kueleza dhulma alizo fanyiwa, ratiba hiyo ilipata mwitikio mkubwa”.

Fahamu kua kituo cha Swidiaqh Twahirah (a.s) kinatoa huduma za kitamaduni na kulinda turathi za Dini katika matukio yoto, kwa kuangalia wakati wa sasa na uliopita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: