Semina elekezi kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Muendelezo wa semina zinazo fanywa na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa watumishi wake, hivi karibuni kitengo kimefanya semina elekezi ya masomo ya Dini na kimaadili, ambayo wameshiriki watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo hicho Shekh Swalahu Karbalai ametuhadithia kuhushu semina hiyo: “Atabatu Abbasiyya inajitahidi kuhakikisha watumishi wake wote wanakua katika ubora mzuri wa kupokea maswali tofauti yanayo ulizwa katika jamii, hususan yanayo husu mambo ya Dini anayo kutana nayo mwanaadamu kila siku”.

Akaongeza kua: “Semina zemepangwa kwa ratiba maalumu ya kila kitengo cha Ataba tukufu, chini ya jopo la masayyid na mashekh watukufu, semina hizi zinaendeshwa kwa njia ya maswali na majibu, njia ambayo ni shirikishi zaidi”.

Akabainisha: “Semina zinahusu mambo muhimu kwa muislamu, anayo kutana nayo kila siku, kama vile swala na mambo yanayo fungamana nayo pamoja na baadhi ya mambo ya kifiqihi”.

Kumbuka kua kitengo cha Dini pamoja na kazi ya kuhudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), vilevile hutoa semina kwa watumishi wa malalo hiyo takatifu, kwa ajili ya kuwawezesha kukabiliana na jambo lolote wanalo weza kukutana nalo ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: