Kikosi cha Answaru Marjaiyya (Liwaau 44/Hashdi Shaábi) kilichopo katika mji wa Hadhar huko Mosul, kwa ajili ya kudhibiti mabaki ya mabaidi wa Daesh, kilicho ongeza idadi ya wapiganai wake siku chache zilizo pita, kamati ya maelekezo na misaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma msafara wa misaada, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake katika mkoa wa Mosul.
Kiongozi wa msafara huo Shekh Haidari Aridhwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu msafara huo: “Kamati ya maelekezo na misaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa misaada kwa wapiganaji waliopo sehemu mbalimali chini ya ratiba maalum, kuanzia wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh na baada yake, leo tumetua katika mkoa wa Mosul kwa ajili ya kugawa zawadi kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (Kuwahudumia ni fahari kwetu)”.
Akaongeza kusema kua: “Kikosi cha opresheni ya Hadhar katika Liwaau Answaru Marjaiyya ni moja ya vituo tulivyo tembelea, tumekutana na kiongozi wa Liwaau hiyo Sayyid Hameed Yasiri pamoja na wapiganaji wake, tumewafikishia salam na dua kutoka kwa Marjaa Dini mkuu, ambaye amewataka wazingatie maelekezo yake na wawe makini kubaini njama za maadui wa Daesh, hali kadhalika tumewafikishia salamu na dua za ndugu zao watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kuwapa zawadi za kutabaruku na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Wapiganaji wamemshukuru Marjaa Dini mkuu kwa kuwapa moyo kupitia misafara mbalimbali anayowatumia kutoka katika Ataba tukufu, wakasema kua msaada wa Marjaa Dini mkuu unawatia moyo zaidi wa kuendelea kupambana na maadui wa Iraq na ubinaadamu.