Miongoni mwa harakati za kongamano la shahada la tisa linalo simamiwa na chama cha Imamu Hussein (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo: (amani ya Fatuma –a.s- ni mwenendo wa wanaislahi), kwa kushirikiana na Ataba tukufu za Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya, Abbasiyya katika mji wa Dabuni mkoani Waasit, kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya maonyesho ya picha za mnato, chini ya anuani isemayo: (Ashura ni alama ya kudumu).
Jumla ya mabango (40) ya picha kutoka nje na ndani ya mkoa wa Karbala yameshiriki, yamechorwa picha zinazo husu harakati ya Imamu Hussein na uhuishaji wa harakati hizo, yakiwemo matembezi yanayo fanywa na mamilioni ya watu pamoja na huduma wanazo pewa mazuwaru wake, hususan katika msimu wa huzuni za Husseiniyya katika mwezi wa –Muharam na Safar- kwa kutumia fani ya uchoraji.
Fahamu kua maonyesho kama haya yamesha wahi kufanywa katika mikoa mingine ya Iraq kabla ya leo, sambamba na kufanywa nje ya Iraq kupitia makongamano mbalimbali ya kimataifa.