Wanafunzi wa Dhiqaar wakiwa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya kupokea ugeni wa wanafunzi, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano na vyuo chini ya kitengo cha uhusiano, imepokea wanafunzi (50) kutoka shule tofauti za mkoa wa Dhiqaar.

Tumeongea na kiongozi wa idara ya mahusiano Ustadh Maahir Khalidi kuhusu ugeni huo, amesema kua: Ugeni huu unatokana na mwaliko wa Atabatu Abbasiyya, wanafunzi wametembezwa katika miradi ya Ataba na wamepewa nasaha za kidini.

Akaongeza kua: “Waliandaliwa ratiba kamili, iliyo husisha kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya pamoja na malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kutembelea makumbusho ya Ataba mbili na mji wa Imamu Hussein (a.s) pamoja na vitalu vya Atabatu Abbasiyya na kituo cha kibiashara cha Al-Afaaf”.

Akaendelea kusema kua: Aidha kulikua na mihadhara mbalimbali kuhusu kujitegemea, uelewa wa jamii na maendeleo, iliyo tolewa na mashekhe tofauti kutoka Atabatu Abbasiyya, wakafafanua vipengele muhimu kutoka kwenye khutuba za swala za Ijumaa ambazo huswaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s).

Wanafunzi wamepongeza mapokezi mazuri waliyo pewa, wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya uhusiano na vyuo, kwa maandalizi mazuri na huduma bora zilizo pambwa na mihadhara mbalimbali.

Kumbuka kua Idara ya mahusiano na vyuo hupokea wanafunzi kutoka vyuo na shule za hapa Iraq kila baada ya muda fulani, na huwatembeza katika miradi yake na huwapa nasaha muhimu kielimu na kitamaduni, yote hayo hufanywa chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel unaosimamiwa na idara tajwa hapo juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: