Kikosi cha usafi chawasili katika eneo linalo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Miongoni mwa kazi ya kusafisha mji mkongwe, watumishi wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu, chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinapiga deki barabara ya Imamu Swadiq (a.s) katika eneo la Baabu-Khaani mashariki ya mji mkongwe, kwa kushirikiana na watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Karbala.

Wamesafisha barabara tajwa pamoja na chochoro zake, kwa kutumia gari maalum za usafi kutoa Atabatu Abbasiyya pamoja na vifaa vingine vya usafi.

Kazi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kudumisha usafi kwenye barabara za mji mkongwe.

Wakazi wa barabara ya Imamu Swadiq (a.s) wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha eneo la katikati ya Ataba mbili tukufu kwa huduma hii, wamesema kua jambo hili sio geni kwa Ataba tukufu, daima imekua ikifanya mambo mbalimbali kwa watu wa mji mkongwe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: