Ni wakwanza kusaidia na bado ni msaada kwa majemedari wa Hashdi Shaábi.

Maoni katika picha
Miongoni mwa msafara maalum wa kuwasaidia wapiganaji wa Hashdi Shaábi katika mji wa Mosul, ujumbe wa maelekezo na misaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya umewasili katika kitongoji cha Fadhiliyya, kutoa misaada kwa wapiganaji.

Tumeongea na kiongozi wa msafara huo Shekh Haidari Aaridhi amesema kua: “Kamati ya misaada na maelekezo inatoa misaada kwa wapiganaji wa Hashdi Shaábi waliopo katika uwanja wa vita, leo tupo katika kitongoji cha Fadhiliyya katika mkoa wa Mosul tukitembelea kituo cha Liwaau/30 Hashdi Shaábi”.

Akaongeza kua: “Tumewafikishia wapiganaji wetu watukufu salamu za Marjaa Dini mkuu pamoja na salamu na dua za ngudu zao watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kuwapa zawadi za kutabaruku na Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na vitu vingine”.

Wapiganaji wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na wasimamizi wake, wakasema hilo sio jambo geni, kwani Atabatu Abbasiyya ilikua ya kwanza kutoa misaada kwa wapiganaji wa Hashdi Shaábi katika maeneo tofauti na bado inaendelea hadi leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: