- Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mashairi ya kiarabu/ juzuu la nne, (yalitolewa majuzuu matatu).
- Nibrasu Anwaru fi Abbasi Akbaru.
- Abbasi mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s) na malalo yake tukufu katika vitabu vya safari za waarabu vilivyo tafsiriwa.
- Atabatu Abbasiyya katika nyaraka za Iraq/ sehemu ya kwanza: ujenzi wa mwaka 1921-1992.
Mkuu wa kituo hicho Shekh Mahmudu Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tangazo la vitabu hivi limetolewa katika nadwa iliyo ratibiwa na kituo, na kuhudhuriwa na jopo la wabobezi wa mambo hayo, wamejadili kitabu hicho na kukitambulisha, pamoja na kutambulisha kazi za kituo na machapisho yake makuu sambamba na mipango yake ya baadae, na kufungua milango ya kusaidiana na kila anayependa”.