Marjaa Dini mkuu amesisitiza kulinda amani ya waandamanaji, ameyasema hayo kwenye khutuba ya Ijumaa (11 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (8 Novemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Shekh Abdulmahdi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Hakika kulinda amani ya waandamanaji ni muhimu sana, jukumu kubwa la kufanikisha hilo lipo chini ya vyombo vya ulinzi na usalama, wanatakiwa wajiepushe kutumia nguvu wanapo amiliana na watu wanaofanya maandamano ya amani, kwani kutumia kwao nguvu hua na matokea mabaya).