Kutoka katika khutuba ya Ijumaa: Baadhi ya athari za kijamii, kielimu, kitamaduni na kiibada zinatokana na umuhimu wa ukweli.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ameongelea baadhi ya athari za kijamii, kielimu na kiibada zinatokana na ukweli, ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa (18 Jamadal-Thani 1441h) sawa na (17 Januari 2020m) iliyo tolewa na mwakilishi wake Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), tumeifupisha katika nukta zifuatazo:

Kwanza: Hakika ukweli huimarisha uaminifu baina ya watu katika mahusiano yao ya kijamii na miamala ya kiuchumi – ukweli wa mtu huifanya jamii ishikamane, isaidiane na ipate utulivu.

Pili: Ili tufanikiwe kijamii, kiuchumi na kitamaduni katika maisha yetu, tunahitaji kushikamana na ukweli – ukweli ni muhimu kwa mwanadini na kwa asiyekua mwanadini, katika jamii ya wachamungu na wasiokua wachamungu, jamii haiwezi kutengemaa ispokua kwa ukweli wa vitendo na kuhadithiwa matukio halisi ya kihistoria na mengineyo.

Tatu: Ukweli ndio hutufanya tuamini ushuhuda wa watu wengine, na kupata mapenzi na ukarimu wao kijamii – hali kadhalika katika uwanja wa kumuabudu Mwenyezi Mungu, mtu mkweli hupendwa na Mwenyezi Mungu.

Nne: Katika zama zetu tunahitaji vyombo vya habari vikweli, waandishi na watangazaji wakweli katika kuelezea historia, matukio na idikadi – tunahitaji daktari mkweli, mhandisi mkweli, mwalimu mkweli – tunahitaji ukweli katika kila sekta ya maisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: