Mheshimiwa Marjaa Dini Ayatullah Shekh Ishaqa Fayadhi asubuhi ya Ijumaa (21 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (17 Desemba 2020m), amemtembelea Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani katika hospitali ya rufaa Alkafeel, kujua maendeleo ya afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji wenye mafanikio chini ya madaktari wa kiiraq hapo jana.
Kumbuka kua Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu alifanyiwa upasuaji kwenye paja la kushoto baada ya kupata tatizo mfupa wa paja hilo, tunamshukuru Mwenyezi Mungu upasuaji ulikua wenye mafanikio.