Hivi punde na muhimu: Tamko la hali ya afya ya Marjaa Dini mkuu.

Maoni katika picha
Siku ya Ijumaa (21 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (17 Januari 2020m) mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ametoa tamko kuhusu hali ya afya ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Hussein Sistani.

Ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kutoka katika ardhi ya Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa baraka zao pamoja na juhudi za jopo la madaktari wa kiiraq wa hospitali ya rufaa Alkafeel, tunawatangazia raia wetu watukufu wa Iraq na umma wa kiislamu kwa ujumla, hakika afya ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani ni nzuri tunamshukuru Allah, inaendelea kuimarika kidogo kidogo.

Jopo la madaktari walio mfanyia upasuaji hapo jana kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu lilifanikiwa, leo afya yake imeimarika kwani ameanza kukaa na ametembea hatua chache, vipimo vya kidaktari vinaonyesha hua hali yake ni nzuri sana, sasa hivi yupo katika uangalizi wa kimatibabu, tunatarajia ataruhusiwa kurudi nyumbani hivi karibuni, pale jopo la madaktari litakapo amua hivyo.

Yafuatayo ni majina ya madaktari walio mfanyia upasuaji Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu katika hospitali ya rufaa Alkafeel:

  • 1- Adnani Issa Karbalai – kiongozi wa jopo la madaktari na bingwa wa mifupa na kuvunjika.
  • 2- Bariri Muhammad Ali Asadiy bingwa wa mifupa na kuvunjika.
  • 3- Ghasani Abdulatifu Yasiri bingwa wa mifupa na kuvunjika.
  • 4- Ihsanu Faraji bingwa wa mifupa na kuvunjika.
  • 5- Ahmadi Ni’matu Twaaiy bingwa wa mifupa na kufunjika.
  • 6- Haitham Asadi bingwa wa mifupa na kuvunjika.
  • 7- Usama Abdulhasan bingwa wa mifupa na kuvunjika.
  • 8- Muhammad Usama mtaalam wa kuondoa hisia kwenye viungo vya mwanaadamu (Takhdiir).
  • 9- Ali Awadi mtaalamu wa kuondoa hisia kwenye viungo vya mwanaadamu (Takhdiir).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: