Idara ya waliopotelewa chini ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya yawatangazia mazuwaru wote waliopoteza vitu vyao wawasiliane nayo kwa namba (07435000393).
Hiyo ndio namba maalum ya kujibu maswali na kutoa maelezo kuhusu vitu vilivyo potea au watu waliopotezana ipo hewani saa (18) kila siku, idara inawataalamu walio bobea na imeandaa taarifa maalum ya kila kilicho botea au kuokotwa.
Kumbuka kua kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu hupokea idadi kubwa ya mazuwaru kila siku na huongezaka zaidi katika siku za ziara maalum na siku za Ijumaa kila wiki, kutokana na idadi hiyo ililazimika kua na idara ya walio potelewa, jukumu la idara hii ni kupokea vitu vilivyo okotwa na kuandika taariza za vitu hivyo, na hukabidhiwa wahusika mara tu baada ya kupatikana kwao, hadi sasa idara imefanikiwa kurudisha vitu vingi vilivyo okotwa kwa wenye navyo na asilimia kubwa ni vitu vya thamani.