Maoni katika picha
Ujenzi unafanywa katika eneo la chuo lenye ukubwa wa mita za mraba (1,113), umepitia hatua tofauti, kunzia uwekaji wa nguzo imara za chuma zilizo tengenezwa katika karakana ya kitengo cha uangalizi wa kihandisi, baada ya kumaliza kuweka nguzo kisha zimejengwa kuta kwa kutumia tofali za block, halafu tumefunga mfumo wa umeme, kila ghorofa lina vyumba (36) vya madarasa, jengo lote lina jumla ya vyumba (144) vilivyo jengwa kisasa, pamoja na kuwepo vyoo kwenye kila ghorofa, sambamba na mitambo ya umeme, mawasiliano na tahadhari, aidha vifaa vyote vya lazima tayali vimesha wekwa.
Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi ni moja ya vitengo muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kina jukumu la kukarabati na kujenga sehemu zote za Ataba tukufu, pamoja na kukarabati na kujenga asilimia kubwa ya miradi inayo simamiwa na Atabatu Abbasiyya sehemu mbalimbali.