Mbele ya malalo ya Saaqi: Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya maombolezo.

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zake za kutoa huduma na kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imepeleka basi zaidi ya 25 katika mji wa Qassim, katika kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Qassim bun Mussa Alkadhim (a.s), hiyo ndio kawaida ya Ataba tukufu katika kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) nje ya mji mtukufu wa Karbala.

Watu wengi wamebebwa na basi hizo kutoka Karbala hadi kwenye mji wa Qassim, kwa ajili ya kuomboleza msiba huo.

Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimewasiliana na idara ya malalo ya Qassim bun Kadhim (a.s) na kuratibu uingiaji wa mawakibu za watu wa Karbala katika mji wa huo, sambamba na kupanga muda wa kuingia na kutoka kwa mawakibu hizo.

Aidha kitengo cha maadhimisho na mawakibu kimefanya maonyesho ya picha chini ya anuani isemayo: (Ashura ni alama ya milele), jumla ya picha (40) kutoka kwa wachoraji wa ndani na nje ya Karbala zimeshiriki katika maonyesho hayo, zikiwepo picha zinazo onyesha maombolezo ya Imamu Hussein (a.s) na matembezi ya mamilioni ya watu pamoja na huduma ambazo hutolewa kwa mazuwaru, hususan wakati wa huzuni za Husseiniyya –Muharam na Safar-.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ndio iliyo sanifu na kutengeneza dirisha la malalo ya Qassim bun Imamu Mussa Alkadhim (a.s), chini ya mafundi wazalendo wa kiwanda cha Saaqi cha kutengeneza madirisha na milango ya makaburi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: