Katika jitihada za kuimarisha utamaduni wa Quráni, Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasyya inafanya vikao vya usomaji wa Quráni sambamba na semina za kufundisha hukumu za tajwidi.
Harakati hazijaishia hapo, bali Maahadi kupitia matawi yake imeamua kuingiza Quráni ndani ya nyumba za watu, hivyo inaendesha visomo vya Quráni ndani ya nyumba za watu, tawi la Maahadi katika wilaya ya Hindiyya limetangaza kufanya kisomo cha Quráni kila wiki ndani ya nyumba ya mmoja wa waumini wake, hukusanyika kundi kubwa la waumini na walimu wa Maahadi pamoja na wanafunzi, na huendeleza kufanya walicho anza kukifanya tangu wiki zilizo pita.
Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, pamoja na kufanya vikao vya usomaji wa Quráni vilevile inafanya semina za kusoma, kuhifadhi na kutafsiri Quráni, hali kadhalika inashirikiana na taasisi zingine za Quráni na kubadilishana uzowefu pamoja na kushiriki katika mashindano na makongamano ya ndani na nje, na inaandaa mubalighina katika sekta ya Quráni kupitia semina za uandaaji wa walimu wa Quráni tukufu.