Idara ya ustawi wa jamii inaendelea kutoa misaada kwenye vituo tofauti.

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ofisi zake zilizopo kwenye mikoa tofauti hapa Iraq, inaendelea kuwasaidia wapiganaji wa Hashdi Shaábi waliopo katika uwanja wa vita, hivi karibuni ofisi ya Tal-Afar imepeleka misaada katika wilaya ya Hadhar Liwaau/25 Hashdi Shaábi katika mkoa wa Mosul.

Msafara huo ulikua na vitu tofauti wanavyo hitaji wapiganaji, vikiwemo vyakula na mavazi.

Wapiganaji wa Liwaau/25 wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya ustawi wa jamii, kwa kutoa misaada kwao bila kusimama tangu ilipotolewa fatwa tukufu ya kujilinda hadi sasa, wakasisitiza kua wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa taifa na Marjaa Dini mkuu na kwamba wao wanafuata maelekezo yake yote, wakamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amponye haraka Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani na adumishe neema na rehema zake kwa taifa la Iraq na raia wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: