Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinashiriki katika opresheni ya kufanya msako upande wa magharibi wa jangwa kwenye eneo lenye ukubwa wa (km 2000).

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kimetangaza ushiriki wake katika opresheni ya kijeshi, inayo lenga kusaka mabaki ya magaidi na wahalifu wanaovunja amani na utulivu wa taifa.

Taarifa imesema kua asubuhi ya leo kikosi kimeshiriki kwenye opresheni kubwa ya Furaat Ausatu kupitia vikosi vyake vya Najafu na Karbala pamoja na Liwaau/33 na Liwaau/16 ya muungano wa wanajeshi na Liwaau ya pili katika kikosi cha Imamu Ali (a.s).

Wakabainisha kua lengo kuu ni kufanya msako katika jangwa la Razaazah kuelekea eneo la Faaji katika mpaka wa mkoa wa Ambaar hadi katika mji wa Nakhiib upande wa mashariki wa mkoa wa Karbala upande wa kusini, na upande wa mpaka wa Najafu kwenye jangwa la kusini.

Ofisi ya kikosi imesema kua wamefanya msako katika eneo lenye ukubwa wa kilometa elfu mbili ya upande wa Nakhiib, kuelekea mpaka wa Iraq na Saudia magharibi ya mkoa wa Karbala na kusini mwa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: