Kuimarisha uhusiano: wanafunzi wa chuo cha Zaharaa (a.s) katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimepokea wanafunzi (50) kutoka chuo cha wasichana cha Zaharaa (a.s) katika mkoa wa Karbala chini ya program ya (kwa pamoja tunajenga maisha ya chuo) inayo lenga kuboresha maisha ya wanafunzi na kuongeza kiwango cha elimu, kituo kimewaandalia ratiba maalum yenye vipengele vingi chini ya wataalam walio bobea.

Mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Ugeni huu umekuja baada ya ushirikiano uliofanywa mwezi wa (12/2019m), wageni wameandaliwa ratiba kamili, inahusisha kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa makundi na kutoa mihadhara miwili, wa kwanza usemao (wewe ni nani?) unao lenga kuwatambulisha wanafunzi umuhimu wa mawasiliano na nguvu ya kua na fikra chanya, na wa pili unasema (uhuru kati ya kukubalika na kutokubalika) unazungumzia maana halisi ya uhuru, na kuheshimu mipaka yake pamoja na namna ya kunufaika nao, sambamba na kuandaa mashindano kwa kuuliza maswali ya Fiqhi, Aqida na mambo mengine, na kutembelea kituo cha kibiashara Al-Afaaf.

Akahitimisha kwa kusema: “Matarajio ya kituo cha utamaduni wa familia ni kuendeleza harakati hizi na kuendelea kupokea wanafunzi pamoja na kuimarisha uhusiano kwa manufaa ya kuhudumia familia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: