Kwa picha: barabara ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika muonekano mpya.

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza kazi ya kutengeneza barabara ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imekua na muonekano mpya unao endana na umuhimu wa barabara hiyo kwa mazuwaru, kwa kiasi ambacho itarahisisha utembeaji wa makundi ya mazuwaru, ukizingatia kua ni barabara kuu inayo elekea katika malalo takatifu na huwa na msongamano mkubwa wa watu hususan wakati wa msimu wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu pamoja na siku za matukio ya Dini.

Hii ni sehemu ya kazi za uboreshaji na itafuatiwa na kazi zingine, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, Mhandisi Samiir Abbasi Ali, akaongeza kua: “Miongoni mwa kazi zilizo kua zikisimamiwa na kitengo hiki ni ujenzi wa barabara ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyokua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Kuweka vizuwizi vyenye upana wa (mt 30) na urefu wa (mt 2) vyenye mapambo mazuri ya kiislamu na vina milango miwili mikubwa inayo saidia kuratibu matembezi ya mazuwaru pamoja na magari.
  • - Kujenga sehemu za kuingilia na kugagulia mazuwaru.
  • - Kujenga mitaro ya maji na kufunga umeme pamoja na kamera za ulinzi na vinginevyo.
  • - Kuondoa lami ya zamani na kuweka ruva za kisasa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 750) pamoja na kuongeza nakshi.
  • - Kutengeneza bustani ya katikati yenye umbo la duara na maua mazuri pamoja na milingoti mitatu iliyo wekwa bendera za Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na bendera ya Iraq”.

Mhandisi bwana Muhammad Mustafa Shaakir Twawiil kiongozi wa idara ya ujenzi katika kitengo tajwa hapo juu, ambao ndio waliofanya ujenzi huu amesema kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inajitahidi kujenga miradi tofauti inayo pendeza kwa watazamaji kwa weledi wa hali ya juu, kazi hii ni sehemu ndogo miongoni mwa kazi zinazo fanywa na kitengo chetu ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kua barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia kazi tofauti za kuiendeleza, ili kuwezesha makundi makubwa ya mazuwaru kutembea kwa urahisi pamoja na magari, kwani ni barabara muhimu inayo elekea katika malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huwa na msongamano mkubwa wa mazuwaru hasa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: