Katika siku kama ya leo (23 Januari) mwaka wa (2017m) Atabatu Abbasiyya tukufu ilizindua kwa mara ya kwanza shamba darasa la aina adimu za tende, hadi leo shamba hilo limefikia ukubwa wa dunam (500), zenye miti ya mitende (9625) na aina (78) zikiwemo tende adimu, bado wanaendelea kufanya tafiti za mbegu kwa ajili ya kupata aina zinazo kubali jangwani.
Aina zilizopo ni: (Barhi Nasiji, Barhi Mahali, Balka, Barim, Amrani, Shawishi, Maktum, Shakkar, Khastawi, Zuhudi, Fahal, Ukhtu Fahal, Twaha Afnadi, Khiyarah, Khadhrawi, Basrawi, Tabruzal Ahmar, Dakal Asghar, Dakal Akhdhar, Sukkari, Abuu Salliy, Ummu Balalizi, Jamali Dini, Khasbah, Baghali, Azraqu Azraqu, Qarnaful, Dahinah, Ashqar, Daklah Ajibah, Burbun, Dairiy, Karkokuliy, Qul Husseiniy, Hilali, Najdiy, Ibrahimiy, Fardhu Abyadhu, Nitatu Saifu, Khulaswah, Halwa Jabal, Fadhwili, Falila, Aswabii Uruus, Majhuul, Hawiiz, Shishi, Nawaadir, biirghudaar, Alanah, Ashrasi, Badarawi, Shamíi, Kantwaar, Aswadu Baidhanjani, Is-haqiy, Saádah, Dajwani, Jadidi, Hamrah Abdu Sayyid, Habru Jamusu, Dakal Aswadu, Khanizi, Zamiliy, Abu Muáni, Jauzi Samawi, Swaáqi).
Tambua kua mradi huu ni sehemu ya kukamilisha mradi mwingine, mradi wa Saaqi wa maji mbadala wa maji ya mto Furaat, ambao unahusisha uchimbaji wa visima katika kupambana na tatizo la ukame na kunufaika na maji ya visima, umeonyesha mafanikio katika umwagiliaji wa mashamba ya mitende.