Kutokana na msimamo wake kuhusu madai ya wananchi wa Iraq, Marjaa Dini mkuu amesisitiza ulazima wa kufanya mabadiliko yanayo daiwa na wananchi, ambayo imekua sababu ya wao kujitolea, aidha amebainisha kua kuchelewa kufanya mabadiliko hayo hakusaidii kitu ispokua ni kuongeza matatizo kwa raia.
Ameyasema hayo kwenye khutuba ya Ijumaa leo (28 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (24 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.
Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Marjaa Dini anasisitiza umuhimu wa kufanya mabadiliko ya kweli ambayo raia wamekua wakiyadai kwa muda mrefu, na wamejitolea mno katika kudai mabadiliko hayo, hakika kuchelewa kutekeleza mabadiliko hayo hakusaidii lolote ispokua kurefusha muda wa kukosekana utulivu wa amani na siasa za taifa).