Marjaa Dini mkuu amesisitiza ulazima wa kuheshimu utawala wa taifa la Iraq na maamuzi yake kisiasa pamoja na umoja wa taifa na raia, na amepinga kila linalo vunja heshima ya taifa kwa aina yeyote.
Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (28 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (24 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.
Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Hakika Marjaa Dini mkuu anasisitiza msimamo wake wa ulazima wa kuheshimu utawala wa Iraq na utulivu wa kisiasa pamoja na umoja wa taifa na raia, na kupinga kila kinacho vunja heshima ya utaifa kwa namna yeyote, wananchi wanauhuru kamili wa kutumia njia za amani na kudai kila wanacho ona kinafaa katika taifa lao bila kuingiliwa na watu wa nje ya taifa).