Marjaa Dini mkuu: ni lazima pande zote zisaidiane kumaliza swala la kuunda serikali ambalo limechelewa sana.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa wito kwa pande zote zishirikiane kuunda serikali mpya na kumaliza tatizo hilo, akasema kufanya hivyo ni hatua muhimu ya kumaliza matatizo ya taifa kwa sasa.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (28 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (24 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi. Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Kuunda serikali mpya kumechukua muda mrefu tofauti na ule uliotajwa kwenye katiba, ni muhimu vikundi vyote visaidiane kumaliza tatizo hili chini ya misingi iliyopangwa, hakika ni hatua muhimu katika kumaliza matatizo yaliyopo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: