Marjaa Dini mkuu: wananchi wa Iraq wanatakiwa kujua ukubwa wa hatari inayo likumba taifa lao na waweke mbele maslahi ya raia.

Maoni katika picha
Kwa mara nyingine Marjaa Dini mkuu amevitaka vikundi vyote vyenye mamlaka na nguvu ya maamuzi, vitambue hatari inayolikumba taifa wakati kwa sasa, na vinatakiwa kua na msimamo mmoja kwa kuangalia maslahi ya taifa na raia.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (28 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (24 Januari 2010m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Hakika Marjaa Dini mkuu anatoa wito kwa vikundi vyoto vya wairaq vitambue hatari inayo likumba taifa lao kwa sasa, wakubaliane kwa pamoja kumaliza hatari hiyo, waweke mbele maslahi ya taifa la Iraq ya sasa na baadae, na Mwenyezi Mungu ni mkuu wa kuwafikisha).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: