Harakati za kiibada kwa wanawake ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa husseiniyya wa kike bado inaendeleza ratiba ya kiibada kila siku ya Ijumaa asubuhi, ambayo ni sehemu ya kunufaika na siku hiyo tukufu kwa kufanya baadhi ya ibada, ikiwa ni pamoja na kusoma dua Nudba iliyo pokewa kutoka kwa Imamu wa zama (a.f).

Bibi Taghrida Tamimi makamo kiongozi wa idara ya makhatibu wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Program hii ni sehemu ya kuonyesha kiapo cha utii kwa Imamu wa zama (a.s), imekua desturi kufanya hivi kila wiki na tunapata mwitikio mkubwa kutoka kwa mazuwari kila Ijumaa.

Akabainisha kua: Ratiba hii huanza kwa muhadhara kisha husomwa dua Nudba na hufatiwa na moja ya dua zilizo pokewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), halafu husomwa dua ya kuliombea taifa la Iraq na raia wake, katika siku za matukio ya kumbukumbu za kuzaliwa au kufariki kwa Maimamu (a.s), huongelewa tukio hilo na huingizwa kwenye ratiba ya siku hiyo.

Kumbuka kua ratiba hii hufanywa kila siku ya Ijumaa asubuhi katika sardabu ya Imamu Hussein (a.s), baada ya kuwajulisha mazuwaru na kuwataka waje kushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: