Miongoni mwa harakati endelevu za Multaqal Qamar chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, ni kutoa mihadhara chini ya anuani isemayo (Akili ya pamoja na habari potofu) katika mkoa wa Bagdad na kuhudhuriwa na makundi tofauti.
Mtoa mada alikua ni mtafiti Ustadh Hassan Aljawadi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye Masjid Rasuulu Aádham (s.a.w.w) na Husseiniyyatu Zaharaa (a.s), katika mada yake amesema kua: “Harakati za Multaqal Qamar zinaendelea katika mikoa tofauti, mihadhara hii ni dalili ya kuendelea kwa harakati hizi ambazo sasa zimetoka Karbala na kuenea mikoa mingine”.
Akaongeza kua: “Tumeangalia namna ya kuamiliana na habari za uongo, na njia za amani tunazo weza kutumia zitakazo tuepusha kushiriki kwenye uongo huo, na kuhakikisha habari hizo hazitangazwi katika jamii kwani huleta fitina na chuki baina ya wananchi”.
Akaendelea kusema: “Tumezuia kwa kiwango kikubwa tatizo la mitandao ya kijamii, ambayo ni sawa na vyanzo vya habari, tumebainisha madhara ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii na namna inavyo weza kusambaza fitna kwa kutangaza habari za uongo”.
Kumbuka kua Multaqal Qamar, ni kongamano la kitamaduni ambalo linalenga makundi tofauti katika jamii, kwa lengo la kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni na kijamii, kwa kutumia njia za kisasa na salama, zisizo jenga chuki wala vurugu mambo ambayo huleta madhara makubwa kwenye jamii.