Kazi hiyo inasimamiwa na kuendeshwa na kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya watumishi walio bobea katika kazi hiyo.
Gari zipo za aina tatu, kuna zinazo beba watu (13) na zinazo beba watu (7) na watu (5) zinafanya kazi muda wote kama ifuatavyo:
- - Kutoka mlango wa Kibla ya Abbasi (a.s) hadi katika uwanja mkuu wa mbele ya barabara ya Jamhuriyya.
- - Kutoka kituo cha barabara ya Alqami hadi katika uwanja wa mbele ya barabara ya Maitham Tammaar.
- - Kutoka kituo cha Qamar hadi Atabatu Husseiniyya tukufu.
Kuna vituo vingine vya muda hupangwa kutokana na mahitaji kwenye ziara kubwa, kwa mfano:
- 1- Kituo cha Qamar hadi mlango wa Bagdad – Alkafeel.
- 2- Kituo cha Hauraa (a.s) hadi mlango wa Bagdad.
Kuna mafundi maaluma wenye jukumu la kuzifanyia matengenezo hizo gari.
Gari hizo haziishii kubeba watu pekeyake, bali zinafanya kazi zingine, katika msimu wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, husaidia kubeba wagonjwa pamoja na kubeba baadhi ya vifaa vya Ataba tukufu, sanjari na kusambaza maji kwa mazuwaru.