Mihadhara elekezi kwa mazuwaru ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zinazo husu mazuwaru wa kike, kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, asubuhi ya Jumamosi kila wiki, hutoa muhadhara ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mbele ya kundi la mazuwaru wa kike.

Huzungumziwa mambo tofauti ya kidini na kiitikadi pamoja na akhlaq na malezi na kila jambo linalo gusa waislamu kwa ujumla hususan wanawake, sambamba na kuambiwa adabu za kufanya ziara, na mwisho hutoa nafasi ya maswali na majibu.

Kumbuka kua kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu hutoa mihadhara ya kidini ndani ya mwaka mzima, pamoja na kufanya majaalisi mbalimbali ndani ya haram ya mnyweshaji wenye kiu Karbala -Saaqi Atwasha Karbala- (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: