Haqibatul-Quráni wameanza mitihani ya mwisho.

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya tawi la mkoa wa Baabil, wameanza kufanya mitihani ya mwisho ya mradi wa Haqibatul-Quráni, mradi unaohusu mada mbili kuu, njia za ufundishaji na Fiqhi.

Mradi huo umepata idadi kubwa ya washiriki kutoka makundi tofauti ya wasomi wa Quráni wanaopenda kuongeza elimu na maarifa ya Quráni tukufu. Mradi wa (Haqibatul-Quráni) unahusisha masomo ya (Maarifa ya Quráni, Tafsiri, Njia za ufundishaji, Sauti na Naghma, Lugha ya kiarabu, Kusimama na kuanza, Uhakiki), masomo hayo yanafundishwa na wakufunzi waliobobea wafuatao:

  • 1- Maarifa ya Quráni (Dokta Riyadhi Rahim Thu’bani).
  • 2- Lugha ya kiarabu (Dokta Hassan Abedi Ma’muri).
  • 3- Njia za ufundishaji (Sayyid Haidari Muhammad Hanai Shallaah).
  • 4- Tafsiri (Dokta Hassan Ma’muri).
  • 5- Sauti na Naghma (Ustadh Muhsin Ramahi).
  • 6- Kusimama na kuanza (Ustadh Nabiil Asadi).
  • 7- Uhakiki (Ustadh Maitham Shaakir Isawi).

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil hufanya mahafali na vikao vingi vya usomaji wa Quráni, pamoja na miradi mbalimbali ya Quráni kama vile nadwa na tafiti za kielimu, kwa ajili ya kufundisha utamaduni wa Quráni katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: