Kitengo cha utalii wa kidini chatangaza ratiba ya safari za kutembelea Ataba tukufu.

Maoni katika picha
Kitengo cha utalii wa kidini chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza ratiba ya safari za kutembelea Ataba na mazaru tukufu za Iraq, kwa bei nafuu na huduma bora tena kwa kutumia gari za kisasa zaidi.

Kwa mujibu wa maelezo ya uongozi wa kitengo hicho, ratiba imepangwa kwa idadi ya siku za wiki kama ifuatavyo:

Jumamosi: Kutembelea watoto wa Muslim bun Aqiil (a.s) pamoja na Atabatu Kadhimiyya, nauli ni (dinari 5000) kwa mtu mmoja, safari itaanza saa moja asubuhi katika mlango wa Bagdad – karibu na bango (screen).

Jumatatu: Kutembelea Atabatu Kadhimiyya pamoja na Atabatu Askariyya na malalo ya Sayyid Muhammad (a.s), nauli ni (dinari 10,000) kwa mtu mmoja, safari itaanza saa kumi na mbili asubuhi katika mlango wa Bagdad – karibu na bango (Screen).

Jumanne: Kutembelea Atabatu Alawiyya na Masjid Kufa pamoja na mazaru zinazo fungamana nazo, sambamba na kutembelea Masjid Sahla, nauli ni (dinari 4000) safari itaanza saa saba Adhuhuri katika mlango wa Bagdad – karibu na bango (Screen).

Ijumaa: Kutembelea Atabatu Kadhimiyya pamoja na Atabatu Askariyya na malalo ya Sayyid Muhammad (a.s), nauli ni (dinari 10,000) kwa mtu mmoja, safari itaanza saa kumi na mbili asubuhi katika mlango wa Bagdad – karibu na bango (screen).

Kitengo kimesema kua nafasi zipo wazi kwa aina zote za safari, na safari ni kwenda na kurudi, kwa kuoda safari au kupata maelezo zaidi fika katika ofisi za kitengo:

  • - Tawi la kwanza/ Mlango wa Bagdad – karibu na kituo cha Alqamar.
  • - Tawi la pili/ Mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Au piga simu kupitia namba zifuatazo: (07602327074/ 07801952463/ 07602283026).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: