Atabatu Abbasiyya tukufu yakanusha taarifa za kujenga hema katika uwanja wa maandamano.

Maoni katika picha
Alasiri ya Jumamosi ya (29 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (25 Januari 2020m) uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kua: “Habari zinazo sambazwa mitandaoni kua Atabatu Abbasiyya tukufu imejenga hema kwenye uwanja wa maandamano mjini Bagdad na mikoa mingine sio za kweli”.

Wakasisitiza kua: “Hakika habari zinazo sambazwa katika mitandao ya kijamii hazina msingi wowote”.

Wakaongeza kua: Ataba inaunga mkono maandamano ya amani ambayo yameruhusiwa na katiba na kupasishwa na Marjaa Dini mkuu, ya kudai islahi na maisha bora.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya inatoa huduma kadhaa kwa waandamanaji, miongoni mwa huduma hizo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula, ambacho hupikwa katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kutumwa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji safi ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa wakati tofauti.
  • - Kutuma gari maalum za usafi pamoja na wasafishaji katika uwanja wa maandamano na maeneo yanayo tumiwa zaidi na waandamanaji.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji ya kunya kwa waandamanaji.
  • - Kutibu watu wanaopata matatizo ya afya kwenye maandamano askari na raia kwa kuwapeleka katika hospitali ya Alkafeel bure.
  • - Kujenga hema la kutoa huduma ya kwanza na kuwafundisha waandamanaji namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi na kila mtu anayepata tatizo la afya kwenye maandamano.
  • - Kutuma misafara ya kusaidia waandamanaji kimkakati kwenye uwanja wa Tahriir mjini Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: