Ofisi ya Samawah chini ya ofisi ya idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kutuma misafara ya kusaidia wapiganaji wa Hashdi Shaábi waliopo katika uwanja wa mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh, kikosi cha Mosul Liwaau/44 Answaru Marjaiyya wanao pambana na mabaki ya magaidi wa Daesh.
Msimamizi wa msafara wamesema kua: “Msafara huu ni sehemu ya misafara mingi ya kutoa misaada iliyotumwa kwenye vikosi tofauti, tumefika hadi kwa wapiganaji wa mji wa Hadhar katika kikosi cha Liwaau Marjaiyya/44 Hashdi Shaábi, msafara huu umebeba bidhaa mbalimbali za chakula na matunda, kwa ajili ya kuwasaidia waendelee kua na msimamo na kudumisha ushindi uliopatikana kwa utukufu wa damu za mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Shaábi”.
Wapiganaji wameshukuru na kusifu juhudi zinazo fanywa na idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya, kwani imekua ikiwasaidia wakati wote bila kuchoka.
Tambua kua idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya inasisitiza kua: “Kutoa misaada ndio kipaombele chetu, kazi yetu inaendelea pamoja na mazingira magumu ambayo taifa linapitia, tunatoa mahitaji yote ya wapiganaji ikiwa ni pamoja na chakula na vinginevyo, misaada hiyo inawasaidia kua na msimamo wa kupambana na kila anayejaribu kuharibu amani ya taifa hili, misaada hiyo ni midogo ukilinganisha na jukumu lao, kuna kauli ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani isemayo: (… Haifai kusahau utukufu wao…), ujumbe huo umefanywa kua kauli mbiu na unatekelezwa kwa vitendo na idara zetu zilizopo kwenye mikoa mingi ya Iraq”.