Kuta za Ataba tukufu na korido zake zimewekwa mapambo meusi, na mabango yaliyo andikwa maneno yanayo ashiria huzuni kutokana na msiba huo.
Kama kawaida Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba kamili ya maombolezo hayo yenye vipengele vifuatavyo:
- - Kufanya majlisi za kuomboleza kuanzia siku ya Jumanne na itaendelea kwa muda wa siku tatu.
- - Kupokea mawakibu za waombolezaji zitakazo kuja kumpa pole Abulfadhil Abbasi kutokana na msiba huu.
- - Kufanya majlisi za kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya mazuwaru.
- - Kufanya majlisi maalum kwa ajili ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya ndani ya ukumbi wa utawala.
- - Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) utagawa chakula kwa mazuwaru watao omboleza msiba huu jirani na haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kumbuka kua wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza kifo cha mtoto wa Mtume Fatuma Zaharaa (a.s). Kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na sehemu lilipo kaburi lake (a.s), inaonyesha namna alivyo dhulumiwa na shida alizo pitia, hadi akamuhusia mme wake kiongozi wa waumini Ali (a.s) afiche kaburi lake wala jeneza lake lisishuhudiwe na yeyote miongoni mwa waliodhulumu haki yake, kwa mujibu wa riwaya nyingi alikufa kishahidi akiwa na umri wa miaka kumi na nane.