Mabango ya kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s) yamewekwa kwenye milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Mlango wa Kibla ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umewekwa kitambaa kikubwa chenye maandishi, kama sehemu ya kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake Zaharaa (a.s) katika msimu huu wa huzuni za Fatwimiyya.

Kitambaa ni moja ya alama za huduni, kina urefu wa (mt 28) na upana wa (mt 6), kimedariziwa kwa uzi mweupe maneno yasemayo (Asalamu alaiki ayyatuha Swidiiqatu Shahiid), pembeni ya maandishi hayo kuna maandishi mengine yasemayo (Yaa Fatwima Zaharaa).

Atabatu Abbasiyya imewekwa mapambo meusi na imetangaza maombolezo kufuatia kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s), zimepandishwa bendera nyeusi na kuwashwa taa nyekundu kama ishara ya kuomboleza na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Kama kawaida ya Ataba tukufu imeandaa ratiba maalum yenye vipengele vingi, kama vile utowaji wa mihadhara ya kidini na kufanya majlisi za uombolezaji, hali kadhalika inapokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala zinazo kuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: