Atabatu Abbasiyya tukufu yapata tuzo mbili katika shindano lililofanywa kwenye kongamano la vitabu vya hauza.

Maoni katika picha
Zaidi ya nakala (1000) za vitabu, Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye mashidhano ya vitabu ya ishirini na moja ambayo hufanywa kila mwaka, katika mji mtukufu wa Qum nchini Iran, na imefanikiwa kupata tuzo mbili kwenye shindano hilo.

Vitabu vilivyo shinda ni:

  • - (Faharasi ya nakalakale za Imamu Khui katika mji wa Najafu) iliyo tolewa na kituo cha upigaji picha nakalakale na fharasi chini ya maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo andaliwa na Ustadh Ahmadi Ali Maajid Alhilliy, yenye juzu mbili: juzu ya kwanza inafaharasi (312) nakala za maandishi, na juzu la pili lina faharasi (288) nakala za maandishi.
  • - (Mausua Rijaliyya cha Allamah Hilliy) kina juzu tano, kimehakikiwa na Ustadh Muhammad Baaqir Malikani, kimetolewa na kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeshawahi kupata tuzo kwenye mashindano haya miaka ya nyuma, hivyo sio mara ya kwanza kupata tuzo hii, pia ni kielelezo cha ubora wa mwenendo wake katika kuhifadhi turathi, kuzihakiki na kuzichapisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: