Atabatu Abbasiyya tukufu yaratibu majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummu Abiiha (a.s).

Maoni katika picha
Kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya majlisi za kuomboleza za jioni kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na kundi la mazuwaru. Mzungumzaji ni Shekh Sharifu Nashi, ameongea kuhusu dhulma aliyo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s), pamoja na namna alivyo jitolea katika kufikisha ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), kisha Sharifu Mula akapanda kwenye mimbari na kusoma majlisi ya kuomboleza.

Tambua kua bibi Zaharaa (a.s) yuko tofauti na maimamu wote watakasifu (a.s), kunariwaya tatu kuhusu tarehe ya kifo chake na zinaombolezwa na waumini kote duniani, hakika yeye ni kiigizo chema kwa wanawake na wanaume, inatosha kua fahari kubwa kwake yeye ni mama wa baba yake (Ummu Abiiha) ndivyo alivyokua akiitwa na mbora wa viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: