Wakina Fatuma wanampa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia mawakibu za kuomboleza kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, wanawake wamekua na nafasi kubwa, kuna mawakibu za wanawake ambazo zimeshiriki kuomboleza kifo cha Swidiiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s) ambae tarehe ya kifo chake inasadifu siku ya kesho Jumatano (3 Jamadal-Aakhar 1441h) kwa mujibu wa riwaya ya tatu kuhusu kifo chake (a.s).

Katika mawakibu ya wanawake kuna makumi ya watu wenye majina ya Fatuma ambao wameshiriki kuomboleza msiba wa mtoto wa Mtume (s.a.w.w), matembezi yameanzia katika haram ya mbeba bendera ya kipenzi wa Zaharaa (a.s) Abulfadhil Abbasi (a.s) kuelekea katika malalo ya ndugu yake Abul-Ahraar (a.s). wakapitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili hadi katika malalo tukufu ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), majonzi na vilio vilitanda kwa mazuwaru hao kutokana na matatizo aliyopata binti wa Mtume (s.a.w.w) na dhulma aliyo fanyiwa baada ya kifo cha baba yake (s.a.w.w), na namna alivyo wakasirikia wale walio mdhulumu.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni’mah Salmani, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Katika kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kuna athari kubwa ndani ya nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), katika msimu wa maombolezo ya Fatwimiyya tumezowea kuona mawakibu za wanawake zikija kutoa pole, kitengo chetu kinaratibu matembezi hayo na kuandaa sehemu maalum ndani ya haram mbili tukufu ya Husseiniyya na Abbasiyya, husimamia harakati yote kwa ujumla kuanzia mwanzo hadi mwisho”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: