Atabatu Abbasiyya imeanza kutengeneza madawati ya shule za Karbala

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza hatua ya kwanza ya kutengeneza madawati kwa lengo la kuyagawa kwenye shule za serikali za mkoa wa Karbala, ili kuziba upungufu uliopo wa madawati, kama sehemu ya kutekeleza mradi wa kusaidia sekta ya malezi na elimu.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi Samiir Abbasi Ali ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu swala hili kua: “Kazi hii ni sehemu ya mchango wa Ataba tukufu katika sekta ya elimu hapa nchini, na kuboresha mazingira ya shule kwa wanafunzi wa ngazi zote, kwa hiyo mafundi wa kitengo chetu wameanza hatua ya kwanza ya kutengeneza madawati karibu (1500) yatakayo sambazwa katika shule za hapa mjini na vijijini”.

Akaongeza kua: Atabatu Abbasiyya imeanza kufanya kazi hiyo kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na umuhimu wa kuboresha mazingira ya elimu katika mikoa tofauti ya Iraq hususan Karbala, sambamba na kuweka mazingira mazuri ya kujisomea kwa wanafunzi, kwa kuwatengenezea madawati bora, kazi hii inafanywa kwa ushirikiano wa kikosi cha Hadaada na (mdf) chini ya idara ya mafundi, baada ya kumaliza utengenezaji wa madawati yatakabidhiwa kwa viongozi wahusika watakao kabidhi shule nufaika kwa makundi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: