Kuhitimisha sehemu ya tatu ya mradi wa Quráni kwa wanafunzi wa Dini

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zinazo lenga kujenga utamaduni wa kushikamana na mafundisho ya Quráni, Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya, imehitimisha sehemu ya tatu ya mradi wa Quráni kwa wanafunzi wa Dini, semina ilikua inahusu usomaji sahihi na hukumu za usomaji wa Quráni hatua ya kwanza, pamoja na maarifa ya Quráni hatua ya pili, wamefundishwa mada tofauti kuhusu Quráni, sambamba na masomo mbalimbali ya hauza.

Semina imefungwa kwa kufanya hafla ya kuhitimu mitihani ya hatua ya kwanza na ya pili, jumla ya washiriki ni zaidi ya wanafunzi (170), raia wa Iraq na wageni, wote wamepewa vyeti vya ushiriki.

Tambua kua mradi huu umepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi wa hauza katika mji wa Najafu, kutokana na faida kubwa inayo patikana katika sekta ya kujifunza utamaduni unaoendana na mafundisho ya Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: