Hospitali ya rufaa Alkafeel imesema kua vyumba vyake vya upasuaji vinaubora wa kimataifa sawa na hospitali za rufaa za nchi zilizo endelea.
Daktari bingwa wa upasuaji Dokta Saamir Faisal amesema kua: “Hospitali ya rufaa Alkafeel inavyumba vya kisasa kabisa vya upasuaji, vinawasukuma mdaktari kufanya upasuaji mkubwa uliokua hauwezi kufanywa zamani hapa Iraq”.
Akasema kua: “Hospitali ya rufaa Alkafeel imesha fanya aina mbalimbali za upasuaji wa kisasa (I.S.O), tofauti na upasuaji wa zamani uliokua unapasua sehemu kubwa ya mwili kwa ajili ya kutibu sehemu yenye tatizo, sasahivi tunatumia njia mbadala kwa vifaa vya kisasa kama vile kiangalia, makoskop na vinginevyo”.