Katika Atabatu Abbasiyya tukufu: Majlisi ya wanawake ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Miguu ya wafuasi wa Ahlulbait imeshindana kwenda katika sardabu ya Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya, kuhudhuria majlisi ya kuomboleza inayo simamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu.

Mazuwaru wakike wamezowea kuhudhuria majlisi hii kila mwaka, huu ni mwaka wa nne mfululizo, katika majlisi hii hufanywa igizo kutokana na riwaya za kuaminika zilizopo kwenye vitabu vya historia zilizo hakikiwa na kuthibitishwa.

Majlisi imepata mahudhurio makubwa ya watu wa rika zote, imefunguliwa kwa Quráni tukufu kisha ikapandishwa bendera ya kuashiria kuanza igizo ambalo maneno yake yanatokana na riwaya zinazo aminika zilizopo kwenye vitabu vya historia.

Kwa maelezo Zaidi kuhusu majlisi hiyo mtandao wa kimataifa Alkafeel umeongea na bibi Taghrida Abdulkhaaliq makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri, amesema kua: “Katika kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s) kutokana na riwaya ya tatu, tunafanya majlisi ya kuomboleza sambamba na igizo linalo onyesha baadhi ya mambo yaliyo mtokea Fatuma Zaharaa (a.s), kwa ajili ya kuwakumbusha wahudhuriaji hali halisi iliyo tokea”.

Akaongeza kua: “Maandalizi ya shughuli hii huchukua karibu miezi mitatu, wanafunzi, watumishi na mubalighina wa idara hii hufanya mazowezi ya igizo, baada ya kuandikwa maneno ya kwenye igizo na kupasishwa na jopo la wataalamu, kisha hugawiwa waigizaji na kuanza kuyafanyia mazowezi”.

Tambua kua idara ya wahadhiri wa kike hufanya harakati mbalimbali katika kukumbuka tukio la furaha au msiba wa Ahlulbait (a.s), kwa namna ambayo inaendana na muhusika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: