Mawakibu za kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha bibi Fatuma (a.s) ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Huzuni na majonzi yametanda na mbingu zinalia kutokana na kuvunjika ubavu wako ewe Swidiiqah Twahirah, hakuna furaha tena katika nyumba ya Mtume baada ya kukukosa, wingu la huzuni na majonzi limetanda, malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imefurika waombolezaji wa kifo cha mtoto wa Mtume (a.s), wamekuja kuhuisha msiba huu mbele ya kaburi lake tukufu, kufuatia kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu), sambamba na kuangalia namna alivyo jitolea mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) na kutaja alivyo dhulumiwa pamoja na kuhimiza kushikamana na misingi ya Ahlulbait (a.s).

Rais wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu maombolezo hayo kua: “Katika msimu wa huzuni za Fatwimiyya unaoitwa (Muharam ndogo) mawakibu huanza kumiminika siku chache kabla ya siku inayosadifu tarehe ya kifo chake, huanza tangu mwezi kumi na tatu ya Jamadal-Uula, na huendelea hadi siku inayotajwa na riwaya ya tatu ambayo ndio siku hizi tulizo nazo”.

Akaongeza kua: “Malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zinapokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala, maombolezo haya yamezoeleka tangu zamani, kitengo chetu kinaratibu matembezi yao, zinaingilia mlango wa mkono (kafu) kutokana na ujenzi unaoendelea katika mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumpa pole huelekea kwenye malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, hushiriki kundi kubwa la mazuwaru katika mawakibu hizo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: