Katika kuhuisha na kukumbuka kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, kutokana na ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu unao umiza roho za wafuasi wa Ahlulbait (a.s), uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, umefanya majlisi maalum ya watumishi wake ndani ya ukumbi wa utawala, ni kawaida yao kufanya hivyo kila kwenye tukio linalo husu watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), tukio hili hupewa umuhimu mkubwa, kuna riwaya tatu zinazotaja kifo chake (a.s).
Majlisi ilifunguliwa kwa kusoma Quráni tukufu, halafu akapanda mimbari Sheikh Muhsin Asadiy kutoka kitengo cha Dini katika Ataba tukufu, ameongea kuhusu nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) kwa baba yake Mtume (s.a.w.w), akasoma hadithi nyingi kuhusu swala hilo, aidha akafafanua mambo ya kihistoria kuhusu msimamo wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kabla ya kuanza kuelezea kifo cha Batuli (a.s) na dhulma kubwa aliyo fanyiwa.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusomwa kaswida na tenzi zinazo elezea msiba huo, ulioacha jeraha kubwa katika nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s) la milele.
Sheikh Swalahu Karbalai rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu maombolezo haya kua: “Nikawaida ya kila jamii kuwakumbuka watukufu wao na viongozi wao wakati wote kwa kufanya mahafali, majlisi na makongamano, kama sehemu ya kuenzi na kuendeleza mema yao, vipi anapokua mtu huyo ni mbora wa wanawake wa duniani wa mwanzo na wa mwisho Zaharaa Albatuul (a.s)? ambae tupo katika siku za kumbukumbu ya kifo chake”.
Akaongeza kua: “Ni heshima kwetu kufanya maombolezo haya na kukumbushana namna alivyo jitolea katika kulinda Dini ya kiislamu, hivyo ni wajibu kwa Ataba ambazo ndio mimbari ya uongofu kuomboleza msiba huu, ikiwemo Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya majlisi na kuendeleza yaliyo fanywa katika maombolezo ya riwaya mbili zilizo pita”.