Mahudhurio makubwa yashuhudiwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Waumini humiminika kutoka vitongoji vya Karbala na miji ya karibu yake katika siku ya Alkhamisi ya kila wiki kwenye malalo ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), haya ndio mazowea ya familia nyingi za wairaq, hali huwa namna gani inapokutana ziara ya usiku wa Ijumaa na tukio lingine la kidini? Mazuwaru hufurika katika uwanja wa katikati ya haram mbili kufanya maadhimisho yote mawili, Ijumaa hii waumini wamefurika katika malalo mawili tukufu kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha bwana wa mashahidi bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya mwisho, hivi sasa tunaishi katika siku hizo tukufu, ambapo utukufu huongezeka mara dufu utakapo fanya ibada karibu na malalo ya bwana wa mashahidi na ndugu yake mbeba bendera (a.s).

Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeboresha mazingira ya kufanya ziara kwa amani na utulivu, katika sehemu za kuswalia na kupumzikia pamoja na huduma bora kutoka kwa watumishi wake, sambamba na kuratibu matembezi ya kuingia na kutoka ndani ya haram tukufu.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya siku za hivi karibuni imeshuhudia makumi ya mawakibu za waomolezaji, pamoja na maelfu ya mazuwaru waliokuja kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Albatuul (a.s) jirani na haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: