Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea kutoa huduma ya chakula kwa mazuwaru chini ya baraka za mkarimu Abulfadhil Abbasi (a.s), kupitia madirisha ya nje ya mgahawa katika siku ya Alkhamisi ya kila wiki, mazuwaru hukichukulia chakula hicho kama dawa kutoka kwa mnyweshaji wenye kiu Karbala (Saaqi Atwaasha Karbala).
Rais wa kitengo cha mgahawa Mhandisi Aadil Hammaami ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Usiku wa Ijumaa ya kila wiki idadi ya mazuwaru huongezeka, huanza kumiminika wakati wa mchana, kwa kiasi ambacho huwa hawana nafasi ya kula chakula cha mchana ndani ya mgahawa (mudhifu), hivyo tukashauriana na ndugu zetu wanaojitolea kufungua madirisha ya nje kwa ajili ya kugawa chakula na vinywaji.
Akaongeza kua: “Baada ya kumaliza kugawa chakula cha mchana huanza kugawa chai na juisi, leo tumeongeza kugawa (mikate ya nyama), baada ya Magharibi tunagawa chakula cha usiku kwa mazuwaru karibu (3000), hua tunaendelea kugawa chakula kwa muda mrefu, tukitarajia kufikisha baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa idadi kubwa zaidi ya mazuwaru”.
Akahitimisha kwa kusema: “Waumini wanaamini kua hukidhiwa mahitaji yao na mwenyezi Mungu kupitia baraka za mkarimu mwezi wa familia (a.s), kutokana na chakula wanacho pewa na mgahawa wake, jambo hilo tumelisikia kwa mazuwaru wengi”.